Tarehe 21 Julai 2025, Mradi wa Pamoja wa Vyama Vikuu vya Ushirika wa Korosho (KCJE) umefanya Mkutano Mkuu wa Nne (4) katika ukumbi wa Shangani Beach Hotel, Mjini Mtwara. Mkutano huo umehusisha viongozi wa vyama vikuu vya ushirika ambao, Warajis Wasaidizi, Wazabuni wa Pembejeo na Magunia, wadau wa sekta ya korosho, Mbaazi na Ufuta pamoja na washirika mbalimbali.
Mkutano huo uliangazia tathmini ya utekelezaji wa shughuli za mradi kwa mwaka uliopita, kupanga mikakati ya mwaka ujao, na kuimarisha ushirikiano kati ya vyama vikuu. Viongozi walisisitiza umuhimu wa uwazi, ushirikiano wa karibu na matumizi sahihi ya rasilimali ili kuinua kilimo cha korosho nchini.
Mgeni rasmi katika mkutano huo alikuwa NANJIVA NZUNDA Ras Msaidizi wa Uchumi na Udhalishaji, ambaye alisisitiza dhamira ya serikali katika kuimarisha sekta ya ushirika. Wengine walioshiriki ni pamoja na Odas O. Mpunga, Mwenyekiti wa Bodi ya KCJE, na wawakilishi kutoka CBT, TPHPA na WMA.
Mradi wa KCJE unaendelea kuwa mfano bora wa ushirikiano miongoni mwa vyama vya ushirika nchini, na kupitia mikutano kama hii, wadau wote wanapata nafasi ya kujifunza, kushirikiana na kuweka mikakati madhubuti kwa maendeleo ya sekta ya korosho na Ushirika Tanzania.